Al-Kahf
Pango (Qur'ani 18), kwa ajili ya Ijumaa
“Atakayesoma sura ya al-Kahf siku ya Ijumaa, nuru itamwangazia kati ya Ijumaa mbili.”
-
بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
Bismillahir-rahmanir-rahim
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.
-
الْحَمْدُ لِلَّهِ الَّذِي أَنزَلَ عَلَىٰ عَبْدِهِ الْكِتَابَ وَلَمْ يَجْعَل لَّهُ عِوَجًا ۜ ١
Al-hamdu lillahil-ladhi anzala 'ala 'abdihil-kitaba wa lam yaj'al lahu 'iwaja
Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, ambaye alimteremshia mja wake Kitabu, wala hakukifanya kuwa na upogo.
-
قَيِّمًا لِّيُنذِرَ بَأْسًا شَدِيدًا مِّن لَّدُنْهُ وَيُبَشِّرَ الْمُؤْمِنِينَ الَّذِينَ يَعْمَلُونَ الصَّالِحَاتِ أَنَّ لَهُمْ أَجْرًا حَسَنًا ٢
Qayyimal-li-yundhira ba'san shadidam-mil-ladunhu wa yubashshiral-mu'mininal-ladhina ya'malunas-salihati anna lahum ajran hasana
Kimenyooka sawa sawa, ili kionye adhabu kali kutoka kwake, na kiwabashirie Waumini watendao mema kwamba hakika wana ujira mzuri.
-
مَّاكِثِينَ فِيهِ أَبَدًا ٣
Makithina fihi abada
Wakae humo milele.
-
وَيُنذِرَ الَّذِينَ قَالُوا اتَّخَذَ اللَّهُ وَلَدًا ٤
Wa yundhiral-ladhina qaluttakhadhallahu walada
Na kiwaonye wasemao, "Mwenyezi Mungu alijifanyia mwana."
-
مَّا لَهُم بِهِ مِنْ عِلْمٍ وَلَا لِآبَائِهِمْ ۚ كَبُرَتْ كَلِمَةً تَخْرُجُ مِنْ أَفْوَاهِهِمْ ۚ إِن يَقُولُونَ إِلَّا كَذِبًا ٥
Ma lahum bihi min 'ilmin wa la li-aba'ihim kaburat kalimatan takhruju min afwahihim in yaquluna illa kadhiba
Wao hawana elimu yoyote ya jambo hili, wala baba zao. Ni neno kubwa hilo litokalo vinywani mwao. Hawasemi isipokuwa uongo tu.
-
فَلَعَلَّكَ بَاخِعٌ نَّفْسَكَ عَلَىٰ آثَارِهِمْ إِن لَّمْ يُؤْمِنُوا بِهَٰذَا الْحَدِيثِ أَسَفًا ٦
Fa-la'allaka bakhi'un nafsaka 'ala atharihim il-lam yu'minu bi-hadhal-hadithi asafa
Huenda ukajihiliki nafsi yako kwa ajili yao, kuwasikitikia kwa kuwa hawayaamini mazungumzo haya!
-
إِنَّا جَعَلْنَا مَا عَلَى الْأَرْضِ زِينَةً لَّهَا لِنَبْلُوَهُمْ أَيُّهُمْ أَحْسَنُ عَمَلًا ٧
Inna ja'alna ma 'alal-ardhi zinatal-laha li-nabluwahum ayyuhum ahsanu 'amala
Kwa hakika tumevifanya vilivyoko juu ya ardhi kuwa ni pambo lake ili tuwafanyie mtihani, ni nani kati yao ndio wenye vitendo vizuri zaidi.
-
وَإِنَّا لَجَاعِلُونَ مَا عَلَيْهَا صَعِيدًا جُرُزًا ٨
Wa inna la-ja'iluna ma 'alaiha sa'idan juruza
Na hakika Sisi tutavifanya vyote vilivyo juu ya ardhi kuwa kama nchi iliyopigwa na ukame.
-
أَمْ حَسِبْتَ أَنَّ أَصْحَابَ الْكَهْفِ وَالرَّقِيمِ كَانُوا مِنْ آيَاتِنَا عَجَبًا ٩
Am hasibta anna ashabal-kahfi war-raqimi kanu min ayatina 'ajaba
Kwani unadhani ya kwamba wale watu wa Pangoni na Maandishi ndio walikuwa tu ajabu miongoni mwa ishara zetu?
-
إِذْ أَوَى الْفِتْيَةُ إِلَى الْكَهْفِ فَقَالُوا رَبَّنَا آتِنَا مِن لَّدُنكَ رَحْمَةً وَهَيِّئْ لَنَا مِنْ أَمْرِنَا رَشَدًا ١٠
Idh awal-fityatu ilal-kahfi fa-qalu rabbana atina mil-ladunka rahmatan wa hayyi' lana min amrina rashada
Vijana hao walipokimbilia kwenye pango, na wakasema, "Mola wetu Mlezi! Tupe rehema itokayo kwako, na tutengezee uongofu katika jambo letu."
-
فَضَرَبْنَا عَلَىٰ آذَانِهِمْ فِي الْكَهْفِ سِنِينَ عَدَدًا ١١
Fa-dharabna 'ala adhanihim fil-kahfi sinina 'adada
Basi tukayaziba masikio yao kuwalaza humo pangoni kwa muda wa miaka kadhaa.
-
ثُمَّ بَعَثْنَاهُمْ لِنَعْلَمَ أَيُّ الْحِزْبَيْنِ أَحْصَىٰ لِمَا لَبِثُوا أَمَدًا ١٢
Thumma ba'athnahum li-na'lama ayyul-hizbaini ahsa lima labithu amada
Kisha tukawazindua ili tujue ni lipi katika makundi mawili yale ndilo lilihesabu sawa zaidi urefu wa muda waliokaa.
-
نَّحْنُ نَقُصُّ عَلَيْكَ نَبَأَهُم بِالْحَقِّ ۚ إِنَّهُمْ فِتْيَةٌ آمَنُوا بِرَبِّهِمْ وَزِدْنَاهُمْ هُدًى ١٣
Nahnu naqussu 'alaika naba'ahum bil-haqqi innahum fityatun amanu bi-rabbihim wa zidnahum huda
Sisi tunakusimulia habari zao kwa haki. Hakika wao walikuwa ni vijana waliomuamini Mola wao Mlezi. Na Sisi tukawazidisha uongofu.
-
وَرَبَطْنَا عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ إِذْ قَامُوا فَقَالُوا رَبُّنَا رَبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ لَن نَّدْعُوَ مِن دُونِهِ إِلَٰهًا ۖ لَّقَدْ قُلْنَا إِذًا شَطَطًا ١٤
Wa rabatna 'ala qulubihim idh qamu fa-qalu rabbuna rabbus-samawati wal-ardhi lan nad'uwa min dunihi ilahal-laqad qulna idhan shatata
Na tukazitia nguvu nyoyo zao waliposimama na wakasema, "Mola wetu Mlezi ni Mola Mlezi wa mbingu na ardhi. Kamwe hatutamuomba mwingine badala yake kuwa ni Mungu. Hivyo, itakuwa tumesema jambo la kuvuka mpaka.
-
هَٰؤُلَاءِ قَوْمُنَا اتَّخَذُوا مِن دُونِهِ آلِهَةً ۖ لَّوْلَا يَأْتُونَ عَلَيْهِم بِسُلْطَانٍ بَيِّنٍ ۖ فَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّهِ كَذِبًا ١٥
Ha'ula'i qawmunattakhadhu min dunihi alihatal-lawla ya'tuna 'alaihim bi-sultanin bayyinin fa-man adhlamu mimmaniftara 'alallahi kadhiba
Hawa kaumu yetu walijifanyia miungu mingine badala yake Yeye. Kwa nini basi hawawatolei uthibitisho ulio dhahiri? Na ni nani aliye dhalimu zaidi kuliko anayemzulia uongo Mwenyezi Mungu?
-
وَإِذِ اعْتَزَلْتُمُوهُمْ وَمَا يَعْبُدُونَ إِلَّا اللَّهَ فَأْوُوا إِلَى الْكَهْفِ يَنشُرْ لَكُمْ رَبُّكُم مِّن رَّحْمَتِهِ وَيُهَيِّئْ لَكُم مِّنْ أَمْرِكُم مِّرْفَقًا ١٦
Wa idhi'tazaltumuhum wa ma ya'buduna illallaha fa'wu ilal-kahfi yanshur lakum rabbukum mir-rahmatihi wa yuhayyi' lakum min amrikum mirfaqa
Na mkijitenga nao na vile wanavyoviabudu badala ya Mwenyezi Mungu, basi kimbilieni pangoni, awafungulie Mola wenu Mlezi katika rehema zake, na awatengenezee ya kuwafaa katika mambo yenu."
-
وَتَرَى الشَّمْسَ إِذَا طَلَعَت تَّزَاوَرُ عَن كَهْفِهِمْ ذَاتَ الْيَمِينِ وَإِذَا غَرَبَت تَّقْرِضُهُمْ ذَاتَ الشِّمَالِ وَهُمْ فِي فَجْوَةٍ مِّنْهُ ۚ
Wa tarash-shamsa idha tala'at tazawaru 'an kahfihim dhatal-yamini wa idha gharabat taqridhuhum dhatash-shimali wa hum fi fajwatim-minh
Na unaliona jua linapochomoza, linainamia kuliani mwao kutoka hapo pangoni, na linapokuchwa, linawakwepa kushotoni, na wao wamo katika uwazi wa pango.
-
ذَٰلِكَ مِنْ آيَاتِ اللَّهِ ۗ مَن يَهْدِ اللَّهُ فَهُوَ الْمُهْتَدِ ۖ
Dhalika min ayatillahi man yahdillahu fa-huwal-muhtad
Hizo ni katika ishara za Mwenyezi Mungu. Yule ambaye Mwenyezi Mungu anamwongoa, basi huyo ameongoka.
-
وَمَن يُضْلِلْ فَلَن تَجِدَ لَهُ وَلِيًّا مُّرْشِدًا ١٧
Wa man yudhlil fa-lan tajida lahu waliyyam-murshida
Na yule ambaye anampoteza, basi hutampatia msimamizi wa kumwongoza.
-
وَتَحْسَبُهُمْ أَيْقَاظًا وَهُمْ رُقُودٌ ۚ وَنُقَلِّبُهُمْ ذَاتَ الْيَمِينِ وَذَاتَ الشِّمَالِ ۖ
Wa tahsabuhum aiqadhan wa hum ruqudun wa nuqallibuhum dhatal-yamini wa dhatash-shimal
Nawe utawadhania wa macho, na hali wamelala. Nasi tunawageuza kulia na kushoto.
-
وَكَلْبُهُم بَاسِطٌ ذِرَاعَيْهِ بِالْوَصِيدِ ۚ لَوِ اطَّلَعْتَ عَلَيْهِمْ لَوَلَّيْتَ مِنْهُمْ فِرَارًا وَلَمُلِئْتَ مِنْهُمْ رُعْبًا ١٨
Wa kalbuhum basitun dhira'aihi bil-wasidi lawittala'ta 'alaihim la-wallaita minhum firaran wa la-muli'ta minhum ru'ba
Na mbwa wao amenyoosha miguu yake ya mbele kizingitini. Kama ungeliwatokea, hakuna shaka ungeligeuka kuwakimbia, huku umejaa hofu kubwa juu yao.
-
وَكَذَٰلِكَ بَعَثْنَاهُمْ لِيَتَسَاءَلُوا بَيْنَهُمْ ۚ قَالَ قَائِلٌ مِّنْهُمْ كَمْ لَبِثْتُمْ ۖ
Wa kadhalika ba'athnahum li-yatasa'alu bainahum qala qa'ilum-minhum kam labithtum
Na kwa namna hiyo tuliwainua usingizini ili wapate kuulizana wao kwa wao. Alisema msemaji katika wao: Mmekaa muda gani?
-
قَالُوا لَبِثْنَا يَوْمًا أَوْ بَعْضَ يَوْمٍ ۚ
Qalu labithna yawman aw ba'dha yawm
Wakasema: Tumekaa siku moja au sehemu ya siku.
-
قَالُوا رَبُّكُمْ أَعْلَمُ بِمَا لَبِثْتُمْ فَابْعَثُوا أَحَدَكُم بِوَرِقِكُمْ هَٰذِهِ إِلَى الْمَدِينَةِ فَلْيَنظُرْ أَيُّهَا أَزْكَىٰ طَعَامًا فَلْيَأْتِكُم بِرِزْقٍ مِّنْهُ وَلْيَتَلَطَّفْ وَلَا يُشْعِرَنَّ بِكُمْ أَحَدًا ١٩
Qalu rabbukum a'lamu bima labithtum fab'athu ahadakum bi-wariqikum hadhihi ilal-madinati falyandhur ayyuha azka ta'aman falya'tikum bi-rizqim-minhu walyatalattaf wa la yush'iranna bikum ahada
Wakasema: Mola wenu Mlezi ndiye anayejua zaidi muda mliokaa. Hebu mtumeni mmoja wenu na hizi fedha zenu aende mjini, akatazame chakula chake kipi kilicho bora kabisa awaletee cha kula. Naye afanye mambo hayo kwa busara, wala kamwe asiwataje kwa yeyote.
-
إِنَّهُمْ إِن يَظْهَرُوا عَلَيْكُمْ يَرْجُمُوكُمْ أَوْ يُعِيدُوكُمْ فِي مِلَّتِهِمْ وَلَن تُفْلِحُوا إِذًا أَبَدًا ٢٠
Innahum in yadhharu 'alaikum yarjumukum aw yu'idukum fi millatihim wa lan tuflihu idhan abada
Kwani wao wakiwatambua, watawapiga mawe, au watawarudisha katika dini yao, na hapo kamwe hamtafanikiwa!
-
وَكَذَٰلِكَ أَعْثَرْنَا عَلَيْهِمْ لِيَعْلَمُوا أَنَّ وَعْدَ اللَّهِ حَقٌّ وَأَنَّ السَّاعَةَ لَا رَيْبَ فِيهَا إِذْ يَتَنَازَعُونَ بَيْنَهُمْ أَمْرَهُمْ ۖ
Wa kadhalika a'tharna 'alaihim li-ya'lamu anna wa'dallahi haqqun wa annas-sa'ata la raiba fiha idh yatanaza'una bainahum amrahum
Na namna hivo ndivyo tulivyowajulisha kwa watu ili wapate kujua ya kwamba ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya kweli, na kwamba Saa haina shaka. Walipokuwa wakigombania jambo lao wao kwa wao,
-
فَقَالُوا ابْنُوا عَلَيْهِم بُنْيَانًا ۖ رَّبُّهُمْ أَعْلَمُ بِهِمْ ۚ
Fa-qalubnu 'alaihim bunyanar-rabbuhum a'lamu bihim
wakasema: Jengeni jengo juu yao. Mola wao Mlezi anawajua vyema.
-
قَالَ الَّذِينَ غَلَبُوا عَلَىٰ أَمْرِهِمْ لَنَتَّخِذَنَّ عَلَيْهِم مَّسْجِدًا ٢١
Qalal-ladhina ghalabu 'ala amrihim la-nattakhidhanna 'alaihim masjida
Wakasema wale walioshinda katika shauri yao: Bila ya shaka tutajenga msikiti juu yao.
-
سَيَقُولُونَ ثَلَاثَةٌ رَّابِعُهُمْ كَلْبُهُمْ وَيَقُولُونَ خَمْسَةٌ سَادِسُهُمْ كَلْبُهُمْ رَجْمًا بِالْغَيْبِ ۖ وَيَقُولُونَ سَبْعَةٌ وَثَامِنُهُمْ كَلْبُهُمْ ۚ
Sa-yaquluna thalathatur-rabi'uhum kalbuhum wa yaquluna khamsatun sadisuhum kalbuhum rajman bil-ghaibi wa yaquluna sab'atun wa thaminuhum kalbuhum
Watasema: Walikuwa watatu, wa nne wao ni mbwa wao. Na wanasema: “Walikuwa watano, wa sita wao ni mbwa wao.ˮ Wanabahatisha ghaibu. Na wanasema: Walikuwa saba, na wa nane wao ni mbwa wao.
-
قُل رَّبِّي أَعْلَمُ بِعِدَّتِهِم مَّا يَعْلَمُهُمْ إِلَّا قَلِيلٌ ۗ
Qur-rabbi a'lamu bi-'iddatihim ma ya'lamuhum illa qalil
Sema: “Mola wangu Mlezi ndiye anayejua sawa sawa hesabu yao. Hawawajui isipokuwa wachache tu.ˮ
-
فَلَا تُمَارِ فِيهِمْ إِلَّا مِرَاءً ظَاهِرًا وَلَا تَسْتَفْتِ فِيهِم مِّنْهُمْ أَحَدًا ٢٢
Fa-la tumari fihim illa mira'an dhahiran wa la tastafti fihim minhum ahada
Basi usibishane juu yao isipokuwa kwa mabishano ya juu juu tu hivi. Wala usiulize habari zao kwa yeyote yule miongoni mwao.
-
وَلَا تَقُولَنَّ لِشَيْءٍ إِنِّي فَاعِلٌ ذَٰلِكَ غَدًا ٢٣
Wa la taqulanna li-shai'in inni fa'ilun dhalika ghada
Wala kamwe usiseme kwa jambo lolote lile: Hakika nitalifanya hilo kesho.
-
إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّهُ ۚ وَاذْكُر رَّبَّكَ إِذَا نَسِيتَ وَقُلْ عَسَىٰ أَن يَهْدِيَنِ رَبِّي لِأَقْرَبَ مِنْ هَٰذَا رَشَدًا ٢٤
Illa an yasha'allahu wadhkur rabbaka idha nasita wa qul 'asa an yahdiyani rabbi li-aqraba min hadha rashada
Isipokuwa Mwenyezi Mungu akipenda. Na mkumbuke Mola wako Mlezi pale unaposahau, na sema: huenda Mola wangu Mlezi ataniongoa kwenye uongozi ulio karibu zaidi kuliko huu.
-
وَلَبِثُوا فِي كَهْفِهِمْ ثَلَاثَ مِائَةٍ سِنِينَ وَازْدَادُوا تِسْعًا ٢٥
Wa labithu fi kahfihim thalatha mi'atin sinina wazdadu tis'a
Na walikaa katika pango lao hilo miaka mia tatu, na wakazidisha tisa.
-
قُلِ اللَّهُ أَعْلَمُ بِمَا لَبِثُوا ۖ لَهُ غَيْبُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ
Qulillahu a'lamu bima labithu lahu ghaibus-samawati wal-ardh
Sema: Mwenyezi Mungu ndiye anayejua zaidi muda waliokaa. Ni zake tu siri za mbingu na ardhi.
-
أَبْصِرْ بِهِ وَأَسْمِعْ ۚ مَا لَهُم مِّن دُونِهِ مِن وَلِيٍّ وَلَا يُشْرِكُ فِي حُكْمِهِ أَحَدًا ٢٦
Absir bihi wa asmi' ma lahum min dunihi min waliyyin wa la yushriku fi hukmihi ahada
Kuona vyema kulikoje kwake na kusikia kuzuri kulikoje! Hawana mlinzi yeyote isipokuwa Yeye, wala hamshirikishi yeyote katika hukumu yake.
-
وَاتْلُ مَا أُوحِيَ إِلَيْكَ مِن كِتَابِ رَبِّكَ ۖ لَا مُبَدِّلَ لِكَلِمَاتِهِ وَلَن تَجِدَ مِن دُونِهِ مُلْتَحَدًا ٢٧
Watlu ma uhiya ilaika min kitabi rabbika la mubaddila li-kalimatihi wa lan tajida min dunihi multahada
Na soma yale uliyofunuliwa katika Kitabu cha Mola wako Mlezi. Hakuna yeyote awezaye kubadilisha maneno yake. Wala nawe hutapata makimbilio yoyote isipokuwa kwake.
-
وَاصْبِرْ نَفْسَكَ مَعَ الَّذِينَ يَدْعُونَ رَبَّهُم بِالْغَدَاةِ وَالْعَشِيِّ يُرِيدُونَ وَجْهَهُ ۖ
Wasbir nafsaka ma'al-ladhina yad'una rabbahum bil-ghadati wal-'ashiyyi yuriduna wajhah
Na isubirishe nafsi yako pamoja na wale wanaomuomba Mola wao Mlezi asubuhi na jioni, hali ya kuwa wanataka uso wake.
-
وَلَا تَعْدُ عَيْنَاكَ عَنْهُمْ تُرِيدُ زِينَةَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ
Wa la ta'du 'ainaka 'anhum turidu zinatal-hayatid-dunya
Wala macho yako yasiwaruke kwa kutaka pambo la uhai wa dunia.
-
وَلَا تُطِعْ مَنْ أَغْفَلْنَا قَلْبَهُ عَن ذِكْرِنَا وَاتَّبَعَ هَوَاهُ وَكَانَ أَمْرُهُ فُرُطًا ٢٨
Wa la tuti' man aghfalna qalbahu 'an dhikrina wattaba'a hawahu wa kana amruhu furuta
Wala usimtii tuliyemghafilisha moyo wake asitukumbuke, na akafuata matamanio yake, na mambo yake yakawa ni kupita tu mipaka.
-
وَقُلِ الْحَقُّ مِن رَّبِّكُمْ ۖ فَمَن شَاءَ فَلْيُؤْمِن وَمَن شَاءَ فَلْيَكْفُرْ ۚ
Wa qulil-haqqu mir-rabbikum fa-man sha'a falyu'min wa man sha'a falyakfur
Na sema: Hii ni haki itokayo kwa Mola wako Mlezi. Basi atakaye, aamini. Na atakaye, akufuru.
-
إِنَّا أَعْتَدْنَا لِلظَّالِمِينَ نَارًا أَحَاطَ بِهِمْ سُرَادِقُهَا ۚ
Inna a'tadna lidh-dhalimina naran ahata bihim suradiquha
Hakika Sisi tumewaandalia madhalimu Moto ambao kuta zake zitawazingira.
-
وَإِن يَسْتَغِيثُوا يُغَاثُوا بِمَاءٍ كَالْمُهْلِ يَشْوِي الْوُجُوهَ ۚ بِئْسَ الشَّرَابُ وَسَاءَتْ مُرْتَفَقًا ٢٩
Wa in yastaghithu yughathu bi-ma'in kal-muhli yashwil-wujuha bi'sash-sharabu wa sa'at murtafaqa
Na wakiomba msaada, watasaidiwa kwa kupewa maji yaliyo kama mafuta yaliyotibuka, yatakayowababua nyuso zao. Ni kinywaji kiovu mno kilichoje hicho, na ni mahali pabaya mno pa kupumzikia palipoje hapo!
-
إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ إِنَّا لَا نُضِيعُ أَجْرَ مَنْ أَحْسَنَ عَمَلًا ٣٠
Innal-ladhina amanu wa 'amilus-salihati inna la nudhi'u ajra man ahsana 'amala
Hakika wale walioamini na wakatenda mema, hakika Sisi hatupotezi ujira wa anayetenda mazuri.
-
أُولَٰئِكَ لَهُمْ جَنَّاتُ عَدْنٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهِمُ الْأَنْهَارُ يُحَلَّوْنَ فِيهَا مِنْ أَسَاوِرَ مِن ذَهَبٍ وَيَلْبَسُونَ ثِيَابًا خُضْرًا مِّن سُندُسٍ وَإِسْتَبْرَقٍ مُّتَّكِئِينَ فِيهَا عَلَى الْأَرَائِكِ ۚ
Ula'ika lahum jannatu 'adnin tajri min tahtihimul-anharu yuhallawna fiha min asawira min dhahabin wa yalbasuna thiyaban khudhram-min sundusin wa istabraqim-muttaki'ina fiha 'alal-ara'ik
Hao watapata Bustani za milele, zinazopita mito kwa chini yao. Humo watapambwa kwa mavazi ya mikononi ya dhahabu, na watavaa nguo za kijani za hariri na atilasi, huku wakiegemea humo juu ya makochi.
-
نِعْمَ الثَّوَابُ وَحَسُنَتْ مُرْتَفَقًا ٣١
Ni'math-thawabu wa hasunat murtafaqa
Hayo ndiyo malipo bora zaidi! Na ndiyo matandiko mazuri mno ya kupumzikia!
-
وَاضْرِبْ لَهُم مَّثَلًا رَّجُلَيْنِ جَعَلْنَا لِأَحَدِهِمَا جَنَّتَيْنِ مِنْ أَعْنَابٍ وَحَفَفْنَاهُمَا بِنَخْلٍ وَجَعَلْنَا بَيْنَهُمَا زَرْعًا ٣٢
Wadhrib lahum mathalar-rajulaini ja'alna li-ahadihima jannataini min a'nabin wa hafafnahuma bi-nakhlin wa ja'alna bainahuma zar'a
Na wapigie mfano wa wanaume wawili: mmoja wao tulimpa vitalu viwili vya mizabibu, na tukavizungushia mitende, na kati yake tukatia mimea ya nafaka.
-
كِلْتَا الْجَنَّتَيْنِ آتَتْ أُكُلَهَا وَلَمْ تَظْلِم مِّنْهُ شَيْئًا ۚ وَفَجَّرْنَا خِلَالَهُمَا نَهَرًا ٣٣
Kiltal-jannataini atat ukulaha wa lam tadhlim minhu shai'an wa fajjarna khilalahuma nahara
Na hivyo vitalu viwili vikatoa mazao yake, wala hapana kitu katika hayo kilichotindikia. Na ndani yake tukapasua mito.
-
وَكَانَ لَهُ ثَمَرٌ فَقَالَ لِصَاحِبِهِ وَهُوَ يُحَاوِرُهُ أَنَا أَكْثَرُ مِنكَ مَالًا وَأَعَزُّ نَفَرًا ٣٤
Wa kana lahu thamarun fa-qala li-sahibihi wa huwa yuhawiruhu ana aktharu minka malan wa a'azzu nafara
Naye alikuwa na mazao mengi. Basi akamwambia mwenzake naye akibishana naye: Mimi nimekushinda wewe kwa mali na nguvu za watu!
-
وَدَخَلَ جَنَّتَهُ وَهُوَ ظَالِمٌ لِّنَفْسِهِ قَالَ مَا أَظُنُّ أَن تَبِيدَ هَٰذِهِ أَبَدًا ٣٥
Wa dakhala jannatahu wa huwa dhalimul-li-nafsihi qala ma adhunnu an tabida hadhihi abada
Na akaingia kitaluni kwake, huku anajidhulumu nafsi yake. Akasema: Sidhani kabisa kuwa haya yatawahi kuharibika milele.
-
وَمَا أَظُنُّ السَّاعَةَ قَائِمَةً وَلَئِن رُّدِدتُّ إِلَىٰ رَبِّي لَأَجِدَنَّ خَيْرًا مِّنْهَا مُنقَلَبًا ٣٦
Wa ma adhunnus-sa'ata qa'imatan wa la'ir-rudittu ila rabbi la-ajidanna khairam-minha munqalaba
Wala sidhani kuwa hiyo Saa (ya Kiyama) itatokea. Na ikiwa nitarudishwa kwa Mola wangu Mlezi, bila ya shaka nitapata marejeo bora zaidi kuliko haya.
-
قَالَ لَهُ صَاحِبُهُ وَهُوَ يُحَاوِرُهُ أَكَفَرْتَ بِالَّذِي خَلَقَكَ مِن تُرَابٍ ثُمَّ مِن نُّطْفَةٍ ثُمَّ سَوَّاكَ رَجُلًا ٣٧
Qala lahu sahibuhu wa huwa yuhawiruhu akafarta bil-ladhi khalaqaka min turabin thumma min nutfatin thumma sawwaka rajula
Mwenzake akamwambia kwa kubishana naye: Je, unamkufuru aliyekuumba kutokana na udongo, tena kutokana na tone la manii, kisha akakufanya mwanamume aliye sawasawa?
-
لَّٰكِنَّا هُوَ اللَّهُ رَبِّي وَلَا أُشْرِكُ بِرَبِّي أَحَدًا ٣٨
Lakinna huwallahu rabbi wa la ushriku bi-rabbi ahada
Lakini Yeye Mwenyezi Mungu ndiye Mola wangu Mlezi. Wala simshirikishi Mola wangu Mlezi na yeyote.
-
وَلَوْلَا إِذْ دَخَلْتَ جَنَّتَكَ قُلْتَ مَا شَاءَ اللَّهُ لَا قُوَّةَ إِلَّا بِاللَّهِ ۚ إِن تَرَنِ أَنَا أَقَلَّ مِنكَ مَالًا وَوَلَدًا ٣٩
Wa lawla idh dakhalta jannataka qulta ma sha'allahu la quwwata illa billahi in tarani ana aqalla minka malan wa walada
Na lau kuwa ulipoingia kitaluni kwako, ungelisema: Mashaallah (alitakalo Mwenyezi Mungu huwa)! Hakuna nguvu yoyote isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu. Ikiwa unaniona mimi nina mali kidogo zaidi na watoto kuliko wewe.
-
فَعَسَىٰ رَبِّي أَن يُؤْتِيَنِ خَيْرًا مِّن جَنَّتِكَ وَيُرْسِلَ عَلَيْهَا حُسْبَانًا مِّنَ السَّمَاءِ فَتُصْبِحَ صَعِيدًا زَلَقًا ٤٠
Fa-'asa rabbi an yu'tiyani khairam-min jannatika wa yursila 'alaiha husbanam-minas-sama'i fa-tusbiha sa'idan zalaqa
Basi huenda Mola wangu Mlezi akanipa kilicho bora kuliko kitalu chako, na akakitumia balaa kutoka mbinguni kwa hivyo kikageuka kuwa ardhi tupu inayoteleza.
-
أَوْ يُصْبِحَ مَاؤُهَا غَوْرًا فَلَن تَسْتَطِيعَ لَهُ طَلَبًا ٤١
Aw yusbiha ma'uha ghawran fa-lan tastati'a lahu talaba
Au maji yake yakazama (katika ardhi), basi usiweze kuyatafuta ukayapata.
-
وَأُحِيطَ بِثَمَرِهِ فَأَصْبَحَ يُقَلِّبُ كَفَّيْهِ عَلَىٰ مَا أَنفَقَ فِيهَا وَهِيَ خَاوِيَةٌ عَلَىٰ عُرُوشِهَا وَيَقُولُ يَا لَيْتَنِي لَمْ أُشْرِكْ بِرَبِّي أَحَدًا ٤٢
Wa uhita bi-thamarihi fa-asbaha yuqallibu kaffaihi 'ala ma anfaqa fiha wa hiya khawiyatun 'ala 'urushiha wa yaqulu ya laitani lam ushrik bi-rabbi ahada
Basi, yakateketezwa matunda yake, akabaki akipinduapindua viganja vyake, kwa vile alivyoyagharamia, huku miti yake imebwagika juu ya chanja zake. Akawa anasema: Laiti nisingelimshirikisha Mola wangu Mlezi na yeyote!
-
وَلَمْ تَكُن لَّهُ فِئَةٌ يَنصُرُونَهُ مِن دُونِ اللَّهِ وَمَا كَانَ مُنتَصِرًا ٤٣
Wa lam takul-lahu fi'atun yansurunahu min dunillahi wa ma kana muntasira
Wala hakuwa na kikundi cha kumnusuru badala ya Mwenyezi Mungu, wala mwenyewe hakuweza kujinusuru.
-
هُنَالِكَ الْوَلَايَةُ لِلَّهِ الْحَقِّ ۚ هُوَ خَيْرٌ ثَوَابًا وَخَيْرٌ عُقْبًا ٤٤
Hunalikal-walayatu lillahil-haqqi huwa khairun thawaban wa khairun 'uqba
Huko ulinzi ni wa Mwenyezi Mungu wa Haki tu. Yeye ndiye mbora zaidi wa malipo, na wa mwisho ulio bora zaidi.
-
وَاضْرِبْ لَهُم مَّثَلَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا كَمَاءٍ أَنزَلْنَاهُ مِنَ السَّمَاءِ فَاخْتَلَطَ بِهِ نَبَاتُ الْأَرْضِ فَأَصْبَحَ هَشِيمًا تَذْرُوهُ الرِّيَاحُ ۗ
Wadhrib lahum mathalal-hayatid-dunya ka-ma'in anzalnahu minas-sama'i fakhtalata bihi nabatul-ardhi fa-asbaha hashiman tadhruhur-riyah
Na wapigie mfano wa uhai wa dunia ambao ni kama maji tunayoyateremsha kutoka mbinguni, yakachanganyika na mimea ya ardhi, kisha mimea hiyo ikawa vibuwa vinavyopeperushwa na upepo.
-
وَكَانَ اللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ مُّقْتَدِرًا ٤٥
Wa kanallahu 'ala kulli shai'im-muqtadira
Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye uweza juu ya kila kitu.
-
الْمَالُ وَالْبَنُونَ زِينَةُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ وَالْبَاقِيَاتُ الصَّالِحَاتُ خَيْرٌ عِندَ رَبِّكَ ثَوَابًا وَخَيْرٌ أَمَلًا ٤٦
Al-malu wal-banuna zinatul-hayatid-dunya wal-baqiyatus-salihatu khairun 'inda rabbika thawaban wa khairun amala
Mali na wana ni pambo la uhai wa dunia. Na mema yanayobakia ni bora mbele ya Mola wako Mlezi kwa malipo, na bora kwa matumaini.
-
وَيَوْمَ نُسَيِّرُ الْجِبَالَ وَتَرَى الْأَرْضَ بَارِزَةً وَحَشَرْنَاهُمْ فَلَمْ نُغَادِرْ مِنْهُمْ أَحَدًا ٤٧
Wa yawma nusayyirul-jibala wa taral-ardha barizatan wa hasharnahum fa-lam nughadir minhum ahada
Na siku tutakapoiondoa milima na ukaiona ardhi iwazi, na tukawafufua, wala hatutamwacha hata mmoja miongoni mwao.
-
وَعُرِضُوا عَلَىٰ رَبِّكَ صَفًّا لَّقَدْ جِئْتُمُونَا كَمَا خَلَقْنَاكُمْ أَوَّلَ مَرَّةٍ ۚ بَلْ زَعَمْتُمْ أَلَّن نَّجْعَلَ لَكُم مَّوْعِدًا ٤٨
Wa 'uridhu 'ala rabbika saffal-laqad ji'tumuna kama khalaqnakum awwala marratin bal za'amtum allan naj'ala lakum maw'ida
Na wakahudhurishwa mbele ya Mola wako Mlezi kwa safu (wakaambiwa): Mmetujia kama tulivyowaumba mara ya kwanza! Bali mlidai kwamba hatutawawekea miadi.
-
وَوُضِعَ الْكِتَابُ فَتَرَى الْمُجْرِمِينَ مُشْفِقِينَ مِمَّا فِيهِ وَيَقُولُونَ يَا وَيْلَتَنَا مَالِ هَٰذَا الْكِتَابِ لَا يُغَادِرُ صَغِيرَةً وَلَا كَبِيرَةً إِلَّا أَحْصَاهَا ۚ
Wa wudhi'al-kitabu fa-taral-mujrimina mushfiqina mimma fihi wa yaquluna ya wailatana mali hadhal-kitabi la yughadiru saghiratan wa la kabiratan illa ahsaha
Na kitawekwa mbele Kitabu. Basi utawaona wahalifu wanavyoogopa mno kwa sababu ya yale yaliyomo. Na watasema: "Ole wetu! Kitabu hiki kina nini! Hakikuacha dogo wala kubwa isipokuwa kililidhibiti vyema?"
-
وَوَجَدُوا مَا عَمِلُوا حَاضِرًا ۗ وَلَا يَظْلِمُ رَبُّكَ أَحَدًا ٤٩
Wa wajadu ma 'amilu hadhiran wa la yadhlimu rabbuka ahada
Na watayakuta yote waliyoyatenda yapo hadharani. Na Mola wako Mlezi hamdhulumu yeyote.
-
وَإِذْ قُلْنَا لِلْمَلَائِكَةِ اسْجُدُوا لِآدَمَ فَسَجَدُوا إِلَّا إِبْلِيسَ كَانَ مِنَ الْجِنِّ فَفَسَقَ عَنْ أَمْرِ رَبِّهِ ۗ
Wa idh qulna lil-mala'ikatisjudu li-Adama fa-sajadu illa Iblisa kana minal-jinni fa-fasaqa 'an amri rabbih
Na tulipowaambia Malaika: Msujudieni Adam! Wakamsjudia isipokuwa Iblisi. Yeye alikuwa miongoni mwa majini, na akavunja amri ya Mola wake Mlezi.
-
أَفَتَتَّخِذُونَهُ وَذُرِّيَّتَهُ أَوْلِيَاءَ مِن دُونِي وَهُمْ لَكُمْ عَدُوٌّ ۚ بِئْسَ لِلظَّالِمِينَ بَدَلًا ٥٠
Afatattakhidhunahu wa dhurriyyatahu awliya'a min duni wa hum lakum 'aduwwun bi'sa lidh-dhalimina badala
Je, mnamchukua yeye na dhuria yake kuwa vipenzi badala yangu, hali wao ni adui zenu? Ni ovu mno badala hii ya madhalimu.
-
مَّا أَشْهَدتُّهُمْ خَلْقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَلَا خَلْقَ أَنفُسِهِمْ وَمَا كُنتُ مُتَّخِذَ الْمُضِلِّينَ عَضُدًا ٥١
Ma ashhattuhum khalqas-samawati wal-ardhi wa la khalqa anfusihim wa ma kuntu muttakhidhal-mudhillina 'adhuda
Sikuwashuhudisha kuumbwa kwa mbingu na ardhi, wala kuumbwa kwa wao wenyewe. Wala sikuwafanya wapotezao kuwa ni wasaidizi.
-
وَيَوْمَ يَقُولُ نَادُوا شُرَكَائِيَ الَّذِينَ زَعَمْتُمْ فَدَعَوْهُمْ فَلَمْ يَسْتَجِيبُوا لَهُمْ وَجَعَلْنَا بَيْنَهُم مَّوْبِقًا ٥٢
Wa yawma yaqulu nadu shuraka'iyal-ladhina za'amtum fa-da'awhum fa-lam yastajibu lahum wa ja'alna bainahum mawbiqa
Na siku atakaposema (Mwenyezi Mungu): Waiteni hao mliodai kuwa ni washirika wangu. Basi watawaita, na wao hawatawaitikia. Nasi tutaweka baina yao maangamio.
-
وَرَأَى الْمُجْرِمُونَ النَّارَ فَظَنُّوا أَنَّهُم مُّوَاقِعُوهَا وَلَمْ يَجِدُوا عَنْهَا مَصْرِفًا ٥٣
Wa ra'al-mujrimunan-nara fa-dhannu annahum muwaqi'uha wa lam yajidu 'anha masrifa
Na wahalifu watauona Moto na watajua ya kwamba wao lazima wataingia humo; wala hawatapata pa kuuepukia.
-
وَلَقَدْ صَرَّفْنَا فِي هَٰذَا الْقُرْآنِ لِلنَّاسِ مِن كُلِّ مَثَلٍ ۚ وَكَانَ الْإِنسَانُ أَكْثَرَ شَيْءٍ جَدَلًا ٥٤
Wa laqad sarrafna fi hadhal-qur'ani lin-nasi min kulli mathalin wa kanal-insanu akthara shai'in jadala
Na bila ya shaka tumewaelezea watu katika Qur-ani hii kila namna ya mfano. Lakini mwanadamu amezidi kuliko kila kitu kwa ubishi.
-
وَمَا مَنَعَ النَّاسَ أَن يُؤْمِنُوا إِذْ جَاءَهُمُ الْهُدَىٰ وَيَسْتَغْفِرُوا رَبَّهُمْ إِلَّا أَن تَأْتِيَهُمْ سُنَّةُ الْأَوَّلِينَ أَوْ يَأْتِيَهُمُ الْعَذَابُ قُبُلًا ٥٥
Wa ma mana'an-nasa an yu'minu idh ja'ahumul-huda wa yastaghfiru rabbahum illa an ta'tiyahum sunnatul-awwalina aw ya'tiyahumul-'adhabu qubula
Na hakikuwazuia watu kuamini ulipowajia uongofu, na kuomba maghfira kwa Mola wao Mlezi, isipokuwa iwafikie desturi ya wale wa mwanzo, au iwafikie adhabu jahara.
-
وَمَا نُرْسِلُ الْمُرْسَلِينَ إِلَّا مُبَشِّرِينَ وَمُنذِرِينَ ۚ وَيُجَادِلُ الَّذِينَ كَفَرُوا بِالْبَاطِلِ لِيُدْحِضُوا بِهِ الْحَقَّ ۖ وَاتَّخَذُوا آيَاتِي وَمَا أُنذِرُوا هُزُوًا ٥٦
Wa ma nursilul-mursalina illa mubashshirina wa mundhirina wa yujadilul-ladhina kafaru bil-batili li-yudhidhu bihil-haqqa wattakhadhu ayati wa ma undhiru huzuwa
Na hatuwatumi Mitume isipokuwa wawe wabashiri na waonyaji. Na wale waliokufuru wanabishana kwa batili, ili kwayo waivunje haki. Na walizifanya Ishara zangu na yale waliyoonywa kuwa ni mzaha.
-
وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّن ذُكِّرَ بِآيَاتِ رَبِّهِ فَأَعْرَضَ عَنْهَا وَنَسِيَ مَا قَدَّمَتْ يَدَاهُ ۚ
Wa man adhlamu mimman dhukkira bi-ayati rabbihi fa-a'radha 'anha wa nasiya ma qaddamat yadah
Na ni nani dhalimu zaidi kuliko yule anayekumbushwa Ishara za Mola wake Mlezi, naye akazipuuza na akasahau yaliyotangulizwa na mikono yake?
-
إِنَّا جَعَلْنَا عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ أَكِنَّةً أَن يَفْقَهُوهُ وَفِي آذَانِهِمْ وَقْرًا ۖ
Inna ja'alna 'ala qulubihim akinnatan an yafqahuhu wa fi adhanihim waqra
Hakika Sisi tumeziba nyoyo zao ili wasifahamu, na uziwi uko kwenye masikio yao.
-
وَإِن تَدْعُهُمْ إِلَى الْهُدَىٰ فَلَن يَهْتَدُوا إِذًا أَبَدًا ٥٧
Wa in tad'uhum ilal-huda fa-lan yahtadu idhan abada
Na ukiwaita kwenye uongofu, kamwe hawataweza kuongoka.
-
وَرَبُّكَ الْغَفُورُ ذُو الرَّحْمَةِ ۖ لَوْ يُؤَاخِذُهُم بِمَا كَسَبُوا لَعَجَّلَ لَهُمُ الْعَذَابَ ۚ بَل لَّهُم مَّوْعِدٌ لَّن يَجِدُوا مِن دُونِهِ مَوْئِلًا ٥٨
Wa rabbukal-ghafuru dhur-rahmati law yu'akhidhuhum bima kasabu la-'ajjala lahumul-'adhaba bal lahum maw'idul-lan yajidu min dunihi maw'ila
Na Mola wako Mlezi ni Msamehevu, Mwenye rehema. Lau angeliwachukulia kwa mujibu wa yale waliyoyachuma, bila ya shaka angeliwafanyia haraka kuwaadhibu. Lakini wanayo miadi ambayo hawatapata makimbilio yoyote ya kuepukana nayo.
-
وَتِلْكَ الْقُرَىٰ أَهْلَكْنَاهُمْ لَمَّا ظَلَمُوا وَجَعَلْنَا لِمَهْلِكِهِم مَّوْعِدًا ٥٩
Wa tilkal-qura ahlaknahum lamma dhalamu wa ja'alna li-mahlikihim maw'ida
Na miji hiyo tuliwaangamiza watu wake walipodhulumu. Na tukawawekea miadi ya maangamizo yao.
-
وَإِذْ قَالَ مُوسَىٰ لِفَتَاهُ لَا أَبْرَحُ حَتَّىٰ أَبْلُغَ مَجْمَعَ الْبَحْرَيْنِ أَوْ أَمْضِيَ حُقُبًا ٦٠
Wa idh qala Musa li-fatahu la abrahu hatta ablugha majma'al-bahraini aw amdhiya huquba
Na pale Musa alipomwambia kijana wake, "Sitaacha kuendelea mpaka nifike zinapokutana bahari mbili, au nitaendelea kwa muda mrefu."
-
فَلَمَّا بَلَغَا مَجْمَعَ بَيْنِهِمَا نَسِيَا حُوتَهُمَا فَاتَّخَذَ سَبِيلَهُ فِي الْبَحْرِ سَرَبًا ٦١
Fa-lamma balagha majma'a bainihima nasiya hutahuma fattakhadha sabilahu fil-bahri saraba
Basi wawili hao walipofika zinapokutana hizo bahari mbili, walimsahau samaki wao, naye akashika njia yake akaponyokea baharini.
-
فَلَمَّا جَاوَزَا قَالَ لِفَتَاهُ آتِنَا غَدَاءَنَا لَقَدْ لَقِينَا مِن سَفَرِنَا هَٰذَا نَصَبًا ٦٢
Fa-lamma jawaza qala li-fatahu atina ghada'ana laqad laqina min safarina hadha nasaba
Walipokwishapita, alimwambia kijana wake: Tupe chakula chetu cha mchana. Kwa hakika tumepata machovu kweli kwa hii safari yetu.
-
قَالَ أَرَأَيْتَ إِذْ أَوَيْنَا إِلَى الصَّخْرَةِ فَإِنِّي نَسِيتُ الْحُوتَ وَمَا أَنسَانِيهُ إِلَّا الشَّيْطَانُ أَنْ أَذْكُرَهُ ۚ
Qala ara'aita idh awaina ilas-sakhrati fa-inni nasitul-huta wa ma ansanihu illash-shaitanu an adhkurah
Akasema (kijana): Unaona! Pale tulipopumzika penye jabali, basi mimi nilimsahau yule samaki. Na hakuna aliyenisahaulisha kumkumbuka isipokuwa Shetani tu.
-
وَاتَّخَذَ سَبِيلَهُ فِي الْبَحْرِ عَجَبًا ٦٣
Wattakhadha sabilahu fil-bahri 'ajaba
Naye akashika njia yake baharini kwa ajabu.
-
قَالَ ذَٰلِكَ مَا كُنَّا نَبْغِ ۚ فَارْتَدَّا عَلَىٰ آثَارِهِمَا قَصَصًا ٦٤
Qala dhalika ma kunna nabghi fartadda 'ala atharihima qasasa
(Musa) akasema: "Hayo ndiyo tuliyokuwa tunayataka." Basi wakarudi nyuma kwa kufuata njia waliyojia.
-
فَوَجَدَا عَبْدًا مِّنْ عِبَادِنَا آتَيْنَاهُ رَحْمَةً مِّنْ عِندِنَا وَعَلَّمْنَاهُ مِن لَّدُنَّا عِلْمًا ٦٥
Fa-wajada 'abdam-min 'ibadina atainahu rahmatam-min 'indina wa 'allamnahu mil-ladunna 'ilma
Basi wakamkuta mja katika waja wetu tuliyempa rehema kutoka kwetu, na tukamfunza mafunzo yaliyotoka kwetu.
-
قَالَ لَهُ مُوسَىٰ هَلْ أَتَّبِعُكَ عَلَىٰ أَن تُعَلِّمَنِ مِمَّا عُلِّمْتَ رُشْدًا ٦٦
Qala lahu Musa hal attabi'uka 'ala an tu'allimani mimma 'ullimta rushda
Musa akamwambia: Nikufuate ili unifunze katika ule uongofu uliofunzwa wewe?
-
قَالَ إِنَّكَ لَن تَسْتَطِيعَ مَعِيَ صَبْرًا ٦٧
Qala innaka lan tastati'a ma'iya sabra
Akasema: Hakika wewe hutaweza kuvumilia kuwa pamoja nami.
-
وَكَيْفَ تَصْبِرُ عَلَىٰ مَا لَمْ تُحِطْ بِهِ خُبْرًا ٦٨
Wa kaifa tasbiru 'ala ma lam tuhit bihi khubra
Na utawezaje kuvumilia yale usiyoyajua vilivyo undani wake?
-
قَالَ سَتَجِدُنِي إِن شَاءَ اللَّهُ صَابِرًا وَلَا أَعْصِي لَكَ أَمْرًا ٦٩
Qala sa-tajiduni in sha'allahu sabiran wa la a'si laka amra
Akasema: In shaa Allah (Mwenyezi Mungu akitaka), utanikuta mvumilivu, wala sitaasi amri yako yoyote.
-
قَالَ فَإِنِ اتَّبَعْتَنِي فَلَا تَسْأَلْنِي عَن شَيْءٍ حَتَّىٰ أُحْدِثَ لَكَ مِنْهُ ذِكْرًا ٧٠
Qala fa-inittaba'tani fa-la tas'alni 'an shai'in hatta uhditha laka minhu dhikra
Akasema: Basi ukinifuata, usiniulize kitu mpaka mimi nianze kukutajia.
-
فَانطَلَقَا حَتَّىٰ إِذَا رَكِبَا فِي السَّفِينَةِ خَرَقَهَا ۖ قَالَ أَخَرَقْتَهَا لِتُغْرِقَ أَهْلَهَا لَقَدْ جِئْتَ شَيْئًا إِمْرًا ٧١
Fantalaqa hatta idha rakiba fis-safinati kharaqaha qala akharaqtaha li-tughriqa ahlaha laqad ji'ta shai'an imra
Basi wawili hao wakatoka, hata walipoabiri jahazi (yule mtu), akalitoboa. (Musa) akasema: Unalitoboa ili uwazamishe watu wake? Hakika umefanya jambo baya mno.
-
قَالَ أَلَمْ أَقُلْ إِنَّكَ لَن تَسْتَطِيعَ مَعِيَ صَبْرًا ٧٢
Qala alam aqul innaka lan tastati'a ma'iya sabra
Akasema: Je, sikusema kwamba wewe hakika hutaweza kuvumilia kuwa pamoja nami?
-
قَالَ لَا تُؤَاخِذْنِي بِمَا نَسِيتُ وَلَا تُرْهِقْنِي مِنْ أَمْرِي عُسْرًا ٧٣
Qala la tu'akhidhni bima nasitu wa la turhiqni min amri 'usra
(Musa) akasema: Usinichukulie makosa kwa niliyosahau, wala usinipe uzito kwa jambo langu.
-
فَانطَلَقَا حَتَّىٰ إِذَا لَقِيَا غُلَامًا فَقَتَلَهُ قَالَ أَقَتَلْتَ نَفْسًا زَكِيَّةً بِغَيْرِ نَفْسٍ لَّقَدْ جِئْتَ شَيْئًا نُّكْرًا ٧٤
Fantalaqa hatta idha laqiya ghulaman fa-qatalahu qala aqatalta nafsan zakiyyatan bi-ghairi nafsil-laqad ji'ta shai'an nukra
Basi wakatoka wawili hao mpaka wakamkuta kijana, akamuua. (Musa) akasema: Ala! Umemuua mtu asiye na kosa, na wala hakuua nafsi yoyote! Ama hakika umefanya jambo baya kabisa!
-
قَالَ أَلَمْ أَقُل لَّكَ إِنَّكَ لَن تَسْتَطِيعَ مَعِيَ صَبْرًا ٧٥
Qala alam aqul laka innaka lan tastati'a ma'iya sabra
(Yule mtu) Akasema, "Je, sikukwambia kwamba hakika wewe hutaweza kusubiri kuwa pamoja nami?"
-
قَالَ إِن سَأَلْتُكَ عَن شَيْءٍ بَعْدَهَا فَلَا تُصَاحِبْنِي ۖ قَدْ بَلَغْتَ مِن لَّدُنِّي عُذْرًا ٧٦
Qala in sa'altuka 'an shai'in ba'daha fa-la tusahibni qad balaghta mil-ladunni 'udhra
(Musa) Akasema, "Nikikuuliza kuhusu kitu chochote baada ya haya, basi usifuatane nami. Kwani hakika umekwishapata udhuru kutoka kwangu."
-
فَانطَلَقَا حَتَّىٰ إِذَا أَتَيَا أَهْلَ قَرْيَةٍ اسْتَطْعَمَا أَهْلَهَا فَأَبَوْا أَن يُضَيِّفُوهُمَا فَوَجَدَا فِيهَا جِدَارًا يُرِيدُ أَن يَنقَضَّ فَأَقَامَهُ ۖ
Fantalaqa hatta idha ataya ahla qaryatinistat'ama ahlaha fa-abaw an yudhayyifuhuma fa-wajada fiha jidaran yuridu an yanqadhdha fa-aqamah
Basi wakaondoka mpaka wakawafikia watu wa mji mmoja. Wakawaomba watu wake wawape chakula, nao wakakataa kuwakaribisha. Hapo wakakuta ukuta unataka kuanguka, (yule mja mwema) akausimamisha.
-
قَالَ لَوْ شِئْتَ لَاتَّخَذْتَ عَلَيْهِ أَجْرًا ٧٧
Qala law shi'ta lattakhadhta 'alaihi ajra
(Musa) akasema, "Ungelitaka, ungelichukua ujira kwa haya."
-
قَالَ هَٰذَا فِرَاقُ بَيْنِي وَبَيْنِكَ ۚ سَأُنَبِّئُكَ بِتَأْوِيلِ مَا لَمْ تَسْتَطِع عَّلَيْهِ صَبْرًا ٧٨
Qala hadha firaqu baini wa bainika sa-unabbi'uka bi-ta'wili ma lam tastati' 'alaihi sabra
(Yule mtu) akasema: Huku ndiko kutengana baina yangu na wewe. Sasa nitakueleza maana ya yale ambayo hukuweza kuyastahamili.
-
أَمَّا السَّفِينَةُ فَكَانَتْ لِمَسَاكِينَ يَعْمَلُونَ فِي الْبَحْرِ فَأَرَدتُّ أَنْ أَعِيبَهَا وَكَانَ وَرَاءَهُم مَّلِكٌ يَأْخُذُ كُلَّ سَفِينَةٍ غَصْبًا ٧٩
Ammas-safinatu fa-kanat li-masakina ya'maluna fil-bahri fa-arattu an a'ibaha wa kana wara'ahum malikun ya'khudhu kulla safinatin ghasba
Ama lile jahazi, hilo lilikuwa la masikini fulani wafanyao kazi baharini. Kwa hivyo, nilitaka kulitia dosari, kwani nyuma yao alikuwapo mfalme aliyekuwa akichukua kwa nguvu majahazi yote.
-
وَأَمَّا الْغُلَامُ فَكَانَ أَبَوَاهُ مُؤْمِنَيْنِ فَخَشِينَا أَن يُرْهِقَهُمَا طُغْيَانًا وَكُفْرًا ٨٠
Wa ammal-ghulamu fa-kana abawahu mu'minaini fa-khashina an yurhiqahuma tughyanan wa kufra
Na ama yule kijana, wazazi wake walikuwa ni Waumini. Tukahofu aje kuwatia mashakani kwa kupindukia mipaka na ukafiri.
-
فَأَرَدْنَا أَن يُبْدِلَهُمَا رَبُّهُمَا خَيْرًا مِّنْهُ زَكَاةً وَأَقْرَبَ رُحْمًا ٨١
Fa-aradna an yubdilahuma rabbuhuma khairam-minhu zakatan wa aqraba ruhma
Basi tulitaka Mola wao Mlezi awabadilishie aliye bora zaidi kuliko huyo kwa kutakasika, na aliye karibu zaidi kwa huruma.
-
وَأَمَّا الْجِدَارُ فَكَانَ لِغُلَامَيْنِ يَتِيمَيْنِ فِي الْمَدِينَةِ وَكَانَ تَحْتَهُ كَنزٌ لَّهُمَا وَكَانَ أَبُوهُمَا صَالِحًا فَأَرَادَ رَبُّكَ أَن يَبْلُغَا أَشُدَّهُمَا وَيَسْتَخْرِجَا كَنزَهُمَا رَحْمَةً مِّن رَّبِّكَ ۚ
Wa ammal-jidaru fa-kana li-ghulamaini yatimaini fil-madinati wa kana tahtahu kanzul-lahuma wa kana abuhuma salihan fa-arada rabbuka an yablugha ashuddahuma wa yastakhrija kanzahuma rahmatam-mir-rabbik
Na ama ukuta ule, huo ulikuwa ni wa vijana wawili mayatima kule mjini. Na chini yake ilikuwapo hazina yao; na baba yao alikuwa ni mtu mwema. Basi Mola wako Mlezi alitaka wafikie utu uzima wao na wajitolee hazina yao wenyewe, hii ikiwa ni rehema itokayo kwa Mola wako Mlezi.
-
وَمَا فَعَلْتُهُ عَنْ أَمْرِي ۚ ذَٰلِكَ تَأْوِيلُ مَا لَمْ تَسْطِع عَّلَيْهِ صَبْرًا ٨٢
Wa ma fa'altuhu 'an amri dhalika ta'wilu ma lam tasti' 'alaihi sabra
Wala mimi sikutenda hayo kwa amri yangu. Hiyo ndiyo tafsiri ya hayo ambayo wewe hukuweza kuyasubiria.
-
وَيَسْأَلُونَكَ عَن ذِي الْقَرْنَيْنِ ۖ قُلْ سَأَتْلُو عَلَيْكُم مِّنْهُ ذِكْرًا ٨٣
Wa yas'alunaka 'an dhil-Qarnaini qul sa-atlu 'alaikum minhu dhikra
Na wanakuuliza kuhusu Dhul-Qarnain. Waambie: nitawasomea baadhi ya hadithi yake.
-
إِنَّا مَكَّنَّا لَهُ فِي الْأَرْضِ وَآتَيْنَاهُ مِن كُلِّ شَيْءٍ سَبَبًا ٨٤
Inna makkanna lahu fil-ardhi wa atainahu min kulli shai'in sababa
Hakika Sisi tulimuimarisha katika ardhi na tukampa katika njia za kila kitu.
-
فَأَتْبَعَ سَبَبًا ٨٥
Fa-atba'a sababa
Basi akaifuata njia.
-
حَتَّىٰ إِذَا بَلَغَ مَغْرِبَ الشَّمْسِ وَجَدَهَا تَغْرُبُ فِي عَيْنٍ حَمِئَةٍ وَوَجَدَ عِندَهَا قَوْمًا ۗ
Hatta idha balagha maghribash-shamsi wajadaha taghrubu fi 'ainin hami'atin wa wajada 'indaha qawma
Mpaka alipofika machweo ya jua, akaliona linatua katika chemichemi yenye matope meusi. Na pale akawakuta kaumu fulani.
-
قُلْنَا يَا ذَا الْقَرْنَيْنِ إِمَّا أَن تُعَذِّبَ وَإِمَّا أَن تَتَّخِذَ فِيهِمْ حُسْنًا ٨٦
Qulna ya dhal-Qarnaini imma an tu'adhdhiba wa imma an tattakhidha fihim husna
Tukasema: Ewe Dhul-Qarnain, ima uwaadhibu au uwafanyie uzuri.
-
قَالَ أَمَّا مَن ظَلَمَ فَسَوْفَ نُعَذِّبُهُ ثُمَّ يُرَدُّ إِلَىٰ رَبِّهِ فَيُعَذِّبُهُ عَذَابًا نُّكْرًا ٨٧
Qala amma man dhalama fa-sawfa nu'adhdhibuhu thumma yuraddu ila rabbihi fa-yu'adhdhibuhu 'adhaban nukra
Akasema: Ama aliyedhulumu, basi tutamuadhibu kisha atarudishwa kwa Mola wake Mlezi, naye atamuadhibu adhabu mbaya zaidi.
-
وَأَمَّا مَنْ آمَنَ وَعَمِلَ صَالِحًا فَلَهُ جَزَاءً الْحُسْنَىٰ ۖ وَسَنَقُولُ لَهُ مِنْ أَمْرِنَا يُسْرًا ٨٨
Wa amma man amana wa 'amila salihan fa-lahu jaza'anil-husna wa sa-naqulu lahu min amrina yusra
Na ama yule mwenye kuamini na akatenda mema, basi huyo ana malipo mazuri, nasi tutamwambia lililo jepesi katika amri yetu.
-
ثُمَّ أَتْبَعَ سَبَبًا ٨٩
Thumma atba'a sababa
Kisha akaifuata njia.
-
حَتَّىٰ إِذَا بَلَغَ مَطْلِعَ الشَّمْسِ وَجَدَهَا تَطْلُعُ عَلَىٰ قَوْمٍ لَّمْ نَجْعَل لَّهُم مِّن دُونِهَا سِتْرًا ٩٠
Hatta idha balagha matli'ash-shamsi wajadaha tatlu'u 'ala qawmil-lam naj'al lahum min duniha sitra
Hata alipofika machomozeo ya jua, akaliona linawachomozea kaumu ambao hatukuwawekea pazia ya kuwakinga kutokana nalo.
-
كَذَٰلِكَ وَقَدْ أَحَطْنَا بِمَا لَدَيْهِ خُبْرًا ٩١
Kadhalika wa qad ahatna bima ladaihi khubra
Vivyo hivyo. Na Sisi tulizijua vilivyo habari zake zote.
-
ثُمَّ أَتْبَعَ سَبَبًا ٩٢
Thumma atba'a sababa
Kisha akaifuata njia.
-
حَتَّىٰ إِذَا بَلَغَ بَيْنَ السَّدَّيْنِ وَجَدَ مِن دُونِهِمَا قَوْمًا لَّا يَكَادُونَ يَفْقَهُونَ قَوْلًا ٩٣
Hatta idha balagha bainas-saddaini wajada min dunihima qawmal-la yakaduna yafqahuna qawla
Hata alipofika katikati ya milima miwili, alikuta nyuma yake kaumu ambao walikaribia kutofahamu neno lolote.
-
قَالُوا يَا ذَا الْقَرْنَيْنِ إِنَّ يَأْجُوجَ وَمَأْجُوجَ مُفْسِدُونَ فِي الْأَرْضِ فَهَلْ نَجْعَلُ لَكَ خَرْجًا عَلَىٰ أَن تَجْعَلَ بَيْنَنَا وَبَيْنَهُمْ سَدًّا ٩٤
Qalu ya dhal-Qarnaini inna Ya'juja wa Ma'juja mufsiduna fil-ardhi fa-hal naj'alu laka kharjan 'ala an taj'ala bainana wa bainahum sadda
Wakasema: Ewe Dhul-Qarnain! Hakika Yaajuju na Maajuju wanafanya uharibifu katika ardhi. Basi je, tukupe ujira ili utie baina yetu na baina yao kizuizi?
-
قَالَ مَا مَكَّنِّي فِيهِ رَبِّي خَيْرٌ فَأَعِينُونِي بِقُوَّةٍ أَجْعَلْ بَيْنَكُمْ وَبَيْنَهُمْ رَدْمًا ٩٥
Qala ma makkanni fihi rabbi khairun fa-a'inuni bi-quwwatin aj'al bainakum wa bainahum radma
Akasema: Yale ambayo Mola wangu Mlezi ameniimarisha ndani yake ndiyo bora zaidi. Lakini nisaidieni kwa nguvu. Nitaweka baina yenu na baina yao kizuizi imara.
-
آتُونِي زُبَرَ الْحَدِيدِ ۖ حَتَّىٰ إِذَا سَاوَىٰ بَيْنَ الصَّدَفَيْنِ قَالَ انفُخُوا ۖ حَتَّىٰ إِذَا جَعَلَهُ نَارًا قَالَ آتُونِي أُفْرِغْ عَلَيْهِ قِطْرًا ٩٦
Atuni zubaral-hadidi hatta idha sawa bainas-sadafaini qalanfukhu hatta idha ja'alahu naran qala atuni ufrigh 'alaihi qitra
Nileteeni vipande vya chuma. Hata alipoijaza sawasawa nafasi iliyo katikati ya milima miwili hiyo, akasema, "Pulizeni moto" mpaka alipokifanya kuwa moto, akasema, "Nileteeni shaba iliyoyeyuka niimimine juu ya chuma hicho."
-
فَمَا اسْطَاعُوا أَن يَظْهَرُوهُ وَمَا اسْتَطَاعُوا لَهُ نَقْبًا ٩٧
Fa-masta'u an yadhharuhu wa mastata'u lahu naqba
Basi hawakuweza kukikwea, wala hawakuweza kukitoboa.
-
قَالَ هَٰذَا رَحْمَةٌ مِّن رَّبِّي ۖ فَإِذَا جَاءَ وَعْدُ رَبِّي جَعَلَهُ دَكَّاءَ ۖ وَكَانَ وَعْدُ رَبِّي حَقًّا ٩٨
Qala hadha rahmatum-mir-rabbi fa-idha ja'a wa'du rabbi ja'alahu dakka'a wa kana wa'du rabbi haqqa
Akasema, "Hii ni rehema kutoka kwa Mola wangu Mlezi. Na itakapokuja ahadi ya Mola wangu Mlezi, atakivunjavunja. Na ahadi ya Mola wangu Mlezi ni ya kweli."
-
وَتَرَكْنَا بَعْضَهُمْ يَوْمَئِذٍ يَمُوجُ فِي بَعْضٍ ۖ وَنُفِخَ فِي الصُّورِ فَجَمَعْنَاهُمْ جَمْعًا ٩٩
Wa tarakna ba'dhahum yawma'idhin yamuju fi ba'dhin wa nufikha fis-suri fa-jama'nahum jam'a
Na tutawaacha baadhi yao siku hiyo wachanganyike wao kwa wao, na litapulizwa baragumu, hapo tutawakusanya wote pamoja.
-
وَعَرَضْنَا جَهَنَّمَ يَوْمَئِذٍ لِّلْكَافِرِينَ عَرْضًا ١٠٠
Wa 'aradhna jahannama yawma'idhil-lil-kafirina 'ardha
Na siku hiyo tutawadhihirishia wazi Jahannamu makafiri waione.
-
الَّذِينَ كَانَتْ أَعْيُنُهُمْ فِي غِطَاءٍ عَن ذِكْرِي وَكَانُوا لَا يَسْتَطِيعُونَ سَمْعًا ١٠١
Alladhina kanat a'yunuhum fi ghita'in 'an dhikri wa kanu la yastati'una sam'a
Wale ambao macho yao yalikuwa paziani hawanikumbuki, na wakawa hawawezi kusikia.
-
أَفَحَسِبَ الَّذِينَ كَفَرُوا أَن يَتَّخِذُوا عِبَادِي مِن دُونِي أَوْلِيَاءَ ۚ إِنَّا أَعْتَدْنَا جَهَنَّمَ لِلْكَافِرِينَ نُزُلًا ١٠٢
Afahasibal-ladhina kafaru an yattakhidhu 'ibadi min duni awliya'a inna a'tadna jahannama lil-kafirina nuzula
Je, wanadhani wale waliokufuru kwamba watawafanya waja wangu kuwa vipenzi wao badala yangu Mimi? Hakika Sisi tumeiandaa Jahannamu iwe ndipo pahali pa kuteremkia pa makafiri.
-
قُلْ هَلْ نُنَبِّئُكُم بِالْأَخْسَرِينَ أَعْمَالًا ١٠٣
Qul hal nunabbi'ukum bil-akhsarina a'mala
Sema: Je, tuwatajieni wenye hasara mno katika vitendo vyao?
-
الَّذِينَ ضَلَّ سَعْيُهُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَهُمْ يَحْسَبُونَ أَنَّهُمْ يُحْسِنُونَ صُنْعًا ١٠٤
Alladhina dhalla sa'yuhum fil-hayatid-dunya wa hum yahsabuna annahum yuhsinuna sun'a
Ni wale ambao juhudi yao katika uhai wa dunia ilipotea bure, nao wanadhani kwamba wanafanya matendo mazuri.
-
أُولَٰئِكَ الَّذِينَ كَفَرُوا بِآيَاتِ رَبِّهِمْ وَلِقَائِهِ فَحَبِطَتْ أَعْمَالُهُمْ فَلَا نُقِيمُ لَهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَزْنًا ١٠٥
Ula'ikal-ladhina kafaru bi-ayati rabbihim wa liqa'ihi fa-habitat a'maluhum fa-la nuqimu lahum yawmal-qiyamati wazna
Hao ni wale waliozikufuru Ishara za Mola wao Mlezi na kukutana naye. Kwa hivyo matendo yao yakapotea bure, na wala Siku ya Kiyama hatutawasimamishia mizani yoyote.
-
ذَٰلِكَ جَزَاؤُهُمْ جَهَنَّمُ بِمَا كَفَرُوا وَاتَّخَذُوا آيَاتِي وَرُسُلِي هُزُوًا ١٠٦
Dhalika jaza'uhum jahannamu bima kafaru wattakhadhu ayati wa rusuli huzuwa
Hayo ndiyo malipo yao, Jahannam, kwa walivyokufuru na wakafanyia stihizai Ishara zangu na Mitume wangu.
-
إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ كَانَتْ لَهُمْ جَنَّاتُ الْفِرْدَوْسِ نُزُلًا ١٠٧
Innal-ladhina amanu wa 'amilus-salihati kanat lahum jannatul-firdawsi nuzula
Hakika wale walioamini na wakatenda mema, mashukio yao yatakuwa kwenye Bustani za Firdausi.
-
خَالِدِينَ فِيهَا لَا يَبْغُونَ عَنْهَا حِوَلًا ١٠٨
Khalidina fiha la yabghuna 'anha hiwala
Watadumu humo; kamwe hawatataka kuondoka humo.
-
قُل لَّوْ كَانَ الْبَحْرُ مِدَادًا لِّكَلِمَاتِ رَبِّي لَنَفِدَ الْبَحْرُ قَبْلَ أَن تَنفَدَ كَلِمَاتُ رَبِّي وَلَوْ جِئْنَا بِمِثْلِهِ مَدَدًا ١٠٩
Qul law kanal-bahru midadal-li-kalimati rabbi la-nafidal-bahru qabla an tanfada kalimatu rabbi wa law ji'na bi-mithlihi madada
Sema: Lau kuwa bahari ingekuwa ndiyo wino kwa maneno ya Mola wangu Mlezi, basi bahari ingelimalizika kabla ya kumalizika maneno ya Mola wangu Mlezi, hata tungeliileta mfano wa hiyo kuongezea.
-
قُلْ إِنَّمَا أَنَا بَشَرٌ مِّثْلُكُمْ يُوحَىٰ إِلَيَّ أَنَّمَا إِلَٰهُكُمْ إِلَٰهٌ وَاحِدٌ ۖ
Qul innama ana basharum-mithlukum yuha ilayya annama ilahukum ilahun wahid
Sema, "Hakika mimi ni mwanadamu tu kama nyinyi. Ninaletewa ufunuo (wahyi) kwamba Mungu wenu ni Mungu Mmoja tu.
-
فَمَن كَانَ يَرْجُو لِقَاءَ رَبِّهِ فَلْيَعْمَلْ عَمَلًا صَالِحًا وَلَا يُشْرِكْ بِعِبَادَةِ رَبِّهِ أَحَدًا ١١٠
Fa-man kana yarju liqa'a rabbihi falya'mal 'amalan salihan wa la yushrik bi-'ibadati rabbihi ahada
Kwa hivyo, mwenye kutaraji kukutana na Mola wake Mlezi, basi na atende matendo mema, wala asimshirikishe yeyote katika ibada ya Mola wake Mlezi."
Qur'ani 18:1-110 · Fadhila: al-Hakim 2/368 (sahihi, al-Albani) · Kutoka kwa Abu Sa'id al-Khudri: “Atakayesoma sura ya al-Kahf siku ya Ijumaa, nuru itamwangazia kati ya Ijumaa mbili.” al-Albani aliipa daraja la sahihi (Sahih al-Jami' 6470); Ibn Hajar aliiita riwaya yenye nguvu zaidi kuhusu al-Kahf. Wengine wanaipokea kama maneno ya Abu Sa'id mwenyewe, kwa “usiku wa Ijumaa” (ad-Darimi); na thawabu kama hii haisemwi kwa maoni, hivyo ina hukumu ya maneno ya Mtume ﷺ; kwa hiyo husomwa kuanzia Magharibi ya Alhamisi hadi Magharibi ya Ijumaa. Aya zake kumi za mwanzo zinamlinda mtu dhidi ya Dajjal (Muslim 809).